Header

“Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo maandiko, ya kuwa alizikwa na alifufuka siku tatu” (1 Wakorintho 15:3-4).

Katika kifungu hiki cha Bibloia mtume Paulo anatueleza kuhusu ujumbe mkuu wa Biblia. Anatuonyesha kwamba katika Biblia kuna mambo ambayo ni yanafaa kupewa umuhimu zaidi. Tunasoma kuhusu mambo haya bi gani. Kwa hivyo Biblia hatufunzi tu kuhusu ujumbe muhimu wa Biblia, bali pia inatufunza pasaka ni nini. Kifungu hiki kinatueleza kwa nini ujumbe wa Biblia ni wa muhimu sana na ni kwa nini tunafaa kuuelewa vyema sana na kuupokea kwa mioyo yetu yote.

1. Pasaka inahusu kifo cha Bwana Yesu Kristo.

Biblia inasema katika kifungu hiki kwamba, “Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yasemavyo maandiko.” Hii inamaanisha kwamba kifo cha Kristo Yesu ndiyo tokeo la muhimu sana katika historia ya ulimwengu wote. Wakati tunasoma Biblia lazima tufahamu kwamba msingi wake wote ni kifo cha Yesu Kristo.

Lazima tukumbuke kwamba Agano la Kale lote linatuongoza kwamba Kristo Yesu na kifo chake. Tukumbuke kwamba waandishi wa Mathayo, Marko, Luka na Yohana, wakati waliandika vitabu hivi, waliandika wakituongoza kwa hili tokea moja, yaani kifo cha Bwana Yesu Kristo. Kila sura ya vitabu hivi vine vya injili, inatuongoza kwa msalaba wa kristo Yesu. Nyaraka za mitume wote msingi wake ni kifo cha Kristo Yesu. Ni kifo cha Kristo Yesu ambacho kiliwaongoza kuandika ujumbe ambao waliandika. Kifo cha Kristo Yesu ndiyo tokeo la maana kabisa.

Katika kifungu hiki tunaelezwa kwamba kifo cha Kristo kiilikuwa kimetabiriwa katika maandiko. Hii inamaanisha kwamba Agano la Kale lote linazungumzia kifo cha Kristo Yesu kama tokeo kuu katika historia ya ulimwengu wote. Hili ni tokeo ambalo lilitabiriwa kwa njia tofauti tofauti katika karne zote. Hili ndilo tokea ambalo Mungu alizungumza kuhusu wakati alimwambia Shetani kwamba, “Atakuponda kichwa, nawe utamgonga kisigino” (Mwanzo 3:15). Hili ndilo tokea ambalo Mungu alikuwa anakudia wakati aliwamuru Waisraeli watoke dhabihu za wanyama katika hekalu. Sheria ya Musa ilitayarisha njia ya kuja kwa kristo Yesu na kifo chake.

Sababu kwa nini kifo cha Kristo Yesu ni cha maana sana ni, kwa sababu kupitia kwa kifo chake, wanadamu waokolewa kutoka kwa dhambi zao. Biblia inasema, “Kristo Yesu alikuja ulimwenguni kuokoa wenye dhambi” (1 Timothy 1:15). Hili ndilo likuwa kusdi la Kristo kuja hapa ulimwenguni: kuwaokoa wenye dhambi kutokana na hatia na uchafu wa dhambi. Kifo chake na kufufuka kwake ndiyo njia ambayo inatuletea wokovu na kutuingiza mbinguni. Bila kifo na kufufuka kwa Kristo Yesu, hakuna wokovu kwa mtu yeyote. Hii ndiyo njia ambayo Mungu ameweka ili sisi tupate kuokoka na ndiyo njia ambayo tunafaa kutumiikiwa tunataka kuokoka.

Ikiwa hujaokoka, utabaki katika dhambi zako hadi utakapokuja kwa Kristo Yesu kwa kumwamini. Utabaki ukiwa hujaokoka hadi utakapoamini katika kifo na kufufuka kwake. Lazima umwombe Mungu akusamehe dhambi zako zote kupitia kwa kifo cha Kristo Yesu msalabani kalvari. Hii ndiyo njia ya pekee ya kupokea msamaha wa dhambi zako, yaani kupitia kwa kifo cha Kristo Yesu msalabani.

2. Pasaka inahusu kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo.

Biblia inasema katika kifungu hiki kwamba, “Kwa maana yale niliyopokea ndiyo niliyowapa ninyi, kama yenye umuhimu wa kwanza: kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama isemavyo maandiko, ya kuwa alizikwa na alifufuka siku ya tatu” (1 Wakorintho 15:3-4).

Kama tu vile kifo cha Kristo Yesu ndiyo msingi wa ujumbe wa injili, vivyo hivyo pia ndivyo ilivyo hata kufufuka kwake. Paulo aliwafundisha Wakorintho kuhusu kifo na kufufuka kwa Kristo Yesu kwa sababu alijua kwamba mambo haya ndiyo msingi wa ujumbe wa injili.

Kufufuka kwa Bwana Yesu Kristo kunamaanisha kwamba Mungu alikubali dhabihu ya Kristo kwa ajili ya watenda dhambi. Msalabani Kalvari Kristo alijitoa kwa ajili ya watenda dhambi na damu yake ili iweze kuwaosha wenye dhambi kutoka kwa dhambi zao. Hivi ndivyo Bwana Yesu kristo alikuwa anafanya msalabani. Alikuwa anafanya kile ambacho makuhani wa Agano la Kale walikuwa wanafanya wakati waliwatoa wanyama kama dhabihu kwa ajili ya watu wote. Walitoa wanayama ambao walikuwa hai ili watu wa Isreali wasihukumiwe na Mungu. Pia walitoa damu ili watu waweze kuoshwa kutoka kwa dhambi zao.

Hivi ndivyo Bwana Yesu Kristo alifanya msalabani Kalvari kwa ajili ya watenda dhambi. Alitoa maisha yake kwa ajili ya dhambi zao na damu yake ili waweze kuoshwa dhambi zao. Kwa hivyo, tunajua kwamba Mungu Baba alikubali dhabihu ya Kristo kwa sababu alimfufua kutoka kwa wafu. Kwa kumfufua kutoka kwa wafu, Mungu Baba alikuwa anasema kwamba yeyote ambaye atamwamini Kristo kwa ajili ya wokovu wake, ataokolewa kutoka katika dhambi zake na kuhakikishiwa nafasi mbinguni. Kwa sababu Kristo Yesu alifufuka, ako na uwezo wa kuwaokoa wote ambao wanakuja kwa Mungu kupitia Yeye (Waebrania 7:25).

Kwa sababu Kristo Yesu alifufuka, ni dhihirisho kwamba Yeye pekee ndiye njia ya wokovu kwa watenda dhambi. Wakati Mungu Baba alimfufua Kristo kutoka kwa wafu, alikuwa anasema kwamba, ni wale tu ambao wanakuja kwake kupitia kwa Kristo ndiyo wataokoka. Kwa sababu ni Yeye ambaye Mungu amempa mamlaka ya kuokoa. Kuna watu wakuu ambao huwapataia watu Fulani mamlaka na husema kwamba ikiwa mtu yeyote anataka kuwaona, lazima mtu apitie kwa mtu au watu hao. Ikiwa mtu hatapitia katika mtu huyu, basi hataweza kumwona mkuu huyo. Kristo ndiye amewekwa na Mungu kuwa Mwokozi wa ulimwengu. Tunajua hili kwa sababu Kristo ndiye amefufuliwa na Mungu. Kufufuka kwa Kristo Yesu si kama kule kwa Lazaro. Lazaro hakupewa mwili mpya ambao haungekufa tena. Baada ya miaka michache baada ya Lazaro kuregeshewa uhai, alikufa tena. Lazaro hauko hai leo katika mwili mpya.

Maana ya Pasaka kwetu leo.

Kwetu leo Pasaka inamaanisha mambo mawili. Inamaanisha kwamba kuna njia ambayo leo tunaweza kupata wokovu. Wanadamu wote ni waovu. Tumezaliwa tukiwa wenye dhambi na tumeishi maisha ya dhambi. Lakini hii haimaanisha kwamba ni lazima tukufe katika dhambi zetu. Mungu ametufungulia njia ambayo tunaweza kupata wokovu. Unawqeza kuwa mtu mwovu sana ambaye ameishi maisha yake yote akitumikia dhambi na uwe hujawahi kuenda kanisani siku hata moja au kufanya jambo lolote zuri. Lakini hii haimaanishi kwamba hakuna tumaini lolote. Ujumbe wa pasaka ni ujumbe wa tumaini. Huu ni ujumbe ambao unatueleza kwamba Mungu amefungua njia kwa watenda dhambi kuja kwake ili waweze kuokoka. Huhitaji kubaki katika dhambi zako, unaweza kuokolewa.

Pili, Pasaka inamaanisha kwamba wale wote ambao watakuja kwa Kristo Yesu kwa kutubu na kwa imani, wamehakikishiwa wokovu. Ikiwa utakuja kwa Kristo Yesu leo na uamue kuacha dhambi zako, ukweli ni kwamba umehakikishiwa msamaha wa dhambi zako nafasi mbinguni. Ikiwa jutakuja kwake leo na umwombe msamaha wa dhambi zako na maisha ya milele mbinguni, atakusikia na atakujibu. Huu ndiyo ujumbe wa pasaka. Ni ujumbe wa tumaini la milele; ni ujumbe kwamba Kristo amaehakikisha wokovu wetu na maisha yetu ya milele.

Hii ndiyo maana halisi ya Pasaka; ni kifo na kufufuka kwa Kristo na ujumbe wa tumaini kwa wote ambao wanatafuta wokovu.